Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wa ECOWAS kujadili hatma ya mzozo wa Guinea leo

Guinea678 Viongozi wa ECOWAS kujadili hatma ya mzozo wa Guinea Leo

Thu, 16 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viongozi wa Afrika Magharibi Ecowas, wanatarajia kujadili mzozo nchini Guinea kufuatia mapinduzi ambao walimg’oa madarakani Rais Alpha Condé,

Taarifa ya kukutana kwa viongozi wa ECOWAS, imetolewa na Wazri wa Mambo ya Nje wa Ghana, Shirley Ayorkor Botchway, kuwa viongozi hao wanakutana leo septemba 16, 2021, kujadili namna ya kuwashinikiza viongozi wa kijeshi kurudisha utawala wa kiraia Ecowas imelaani mapinduzi na tayari imeiondoa katika uanachama wake.

"Marais wataangalia ripoti na kuamua nini la kufanya. Wataamua kuhusu jinsi ya kuwawekea waliofanya mapinduzi ili kuirejesha Guinea tena katika utawala wa kikatiba ," amesema Botchway.

Hata hivyo Jumuiya hiyo imetuma ujumbe wa kukutana na viongozi wa jeshi la mapinduzi kwa ajili ya kujadili muafaka wa yanayoendelea katika taifa hilo ikiwa ni pamoja na kushinikiza kuachiwa kwa rais Conde.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live