Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi EAC wawasili Kenya kujadili mzozo wa Rwanda na Congo

EAC FLKAG KENYA Viongozi EAC wawasili Kenya kujadili mzozo wa Rwanda na Congo

Mon, 20 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viongozi wa mataifa saba yanayounda Jumuiya ya Afrika Mashariki wanatarajiwa kukutana kujadili hali ya usalama katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kulingana na taarifa ya serikali.

Viongozi hao wanakutana kwa mualiko wa mwenyeji wao Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya hiyo.

Muda mfupi uliopita Rais wa Uganda Yoweri Museveni amethibitisha kwenye mtandao wake rasmi wa Twitter kwamba amewasili jijini Nairobi kkuhudhuria Kikao cha Tatu cha Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live