Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi Afrika Mashariki wanakutana Burundi kujadili hali ya usalama DRC

Viongozi Afrika Mashariki Wanakutana Burundi Kujadili Hali Ya Usalama DRC Viongozi Afrika Mashariki wanakutana Burundi kujadili hali ya usalama DRC

Sat, 4 Feb 2023 Chanzo: Bbc

Viongozi wa mataifa ya Afrika Mashariki wanakutana nchini Burundi leo Jumamosi kujadili mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Mkutano huo unafanyika siku moja baada ya Papa Francis kutoa wito wa kusitishwa mapigano wakati akikamilisha ziara yake ya siku tatu nchini humo.

Mapigano yameendelea kushuhudiwa hata wakati wa ziara yake kingozi huyo mkuu wa kanisa katoliki, huku watu kadhaa wakiripotiwa kuuawa katika siku chache zilizopita katika mapigano kati ya vikosi vya serikali na makundi ya waasi.

Mkuatno huo wa viongozi wakuu wa serikali kutoka jumuiya ya Afrika mashariki wakati mpaigano yanaendelea Kivu ya kaskazini. Waasi wa M23 wanautuhumiwa kuhusika na ghasia zinazoshuhudiwa wakati katika wiki za hivi karibuni waasi hao wamedhibiti miji iliopo mashariki mwa Congo.

Kunid hilo linashutumiwa kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mpaigano yalionuiwa kutoa fursa ya mazungumzo ya kusitisha ghasia hizo.

Wasiwasi unaoongezeka kati ya Congo na Jirani yake Rwanda pia utajadiliwa katika kikao cha viongozi hao wa kanda.

Jumuiya ya Afrika mashariki imetuma wanajeshi ndani ya Congo kuvisadia vikosi vya serikali na walind aamani wa Umoja wa mataifa kupambana na makundi kadhaa yaliojihami yanayohudumu mashariki mwa nchi hiyo.

Mamia ya watu wameuawa na wengine zaidi ya laki nne wametoroka makaazi yao kufuatia mapigano katika eneo hilo lenye utajiri wa madini.

Chanzo: Bbc