Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi 5 wa Afrika ambao baba zao walikuwa Marais

Cfbe145bfbc543fb Viongozi 5 wa Afrika ambao baba zao walikuwa Marais

Mon, 27 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Utamaduni wa kukabidhi mamlaka kutoka kizazi kimoja hadi kingine ni sehemu ya tabia ya KiafrikaTabia hii ya muda mrefu inaonekana katika nyakati za siasa za kisasa Afrika ambapo serikali huchaguliwa kuwa madarakani katika mazingira ya kidemokrasiaKatika mataifa mengine ya Kiafrika mfano Gabon, Togo, na Kongo, kumekuwa na visa ambapo akina baba huwavisha vazi la uongozi watoto wao ilivyokuwa zamaniMarais wengi wa Kiafrika wanashikilia ofisi ambazo ziliwahi kukaliwa na wazazi wao katika miaka ya nyuma.

Hapa ni orodha ya marais wa Kiafrika ambao baba zao pia walikuwa marais:

1. Uhuru Kenyatta na Jomo Kenyatta (Kenya)Uhuru Kenyatta, mtoto wa Jomo Kenyatta, ndiye rais wa sasa wa Kenya.

Mzee Jomo Kenyatta ndiye baba mwanzilishi na rais wa kwanza wa Jamhuri ya Kenya aliyetawala kutoka uhuru hadi mwaka wa 1978 alipofariki dunia.

Mwanawe, Uhuru, angechukua hatamu za uongozi wa nchi miaka 35 baadaye.

Uhuru alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuingia Ikulu mnamo mwaka wa 2013 wakati aliposhirikiana na William Ruto ambaye amekuwa naibu wake tangu hapo.

Aligombea urais tena mnamo 2017 ambapo alishinda dhidi ya mpinzani wake, waziri mkuu wa zamani Raila Odinga.

Kura hiyo ilikumbwa na utata na ushindi wa Uhuru ukatupiliwa mbali na Mahakama ya Juu Zaidi, ilitaja kasoro za uchaguzi kuwa sababu ya kubatilisha ushindi huo.

Korti iliamuru uchaguzi mpya kufanywa ambao Raila hakushiriki, na kumpa Uhuru ushindi rahisi.

Uhuru atakuwa anamaliza muda wake mwaka 2022 wakati uchaguzi mkuu ujao utakapofanyika.

2. Edward Akufo-Addo na Nana Akufo-Addo (Ghana)Rais Nana Akufo-Addo amekuwa madarakani tangu Januari 7, 2017. Baba yake, Edward Akufo-Addo, alikuwa kiongozi asiye na amri nchini humo kutoka mwaka wa 1970 hadi 1972, baada ya kuwa jaji mkuu wa tatu (1966-1970).

3. Ali Bongo na Omar Bongo (Garbon)Mnamo 2009, Rais Ali Bongo alichukua uongozi wa Garbon kutoka kwa baba yake marehemu, Omar Bongo, ambaye alikuwa ofisini tangu 1967. Baada ya kifo cha baba yake, Ali alichaguliwa mnamo 2009 na akachaguliwa tena mnamo 2016.

4. Faure Gnassingbe Eyadema na Gnassingbe Eyadema (Togo)Faure Gnassingbe Eyadema aliwekwa mara moja kuwa rais wa Togo mnamo 2005 kufuatia kifo cha baba yake, Gnassingbe Eyadema, mwaka huo huo. Gnassingbe aliongoza nchi hiyo kutoka 1967 hadi 2005.

5. Joseph Kabila na Laurent-Desire Kabila (Congo)Chini ya mwezi mmoja baada ya mauaji ya marehemu Rais Laurent-Desire Kabila mnamo 2001, mtoto wake, Joseph Kabila, alichukua madaraka. Baadaye alichaguliwa mnamo 2006 na akachaguliwa tena mnamo 2011. Kulingana na katiba ya 2006 ya Jamhuri ya Demokrasiasa ya Congo (DRC), rais wa zamani atasalia kuwa seneta hadi afe.

Mchango wake Raphael Abuna, Mwalimu Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Igunga

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke