Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vilio vyatanda Cameroon maporomoko ya ardhi yakitokea

Cameroon Maporomoko (600 X 305) Vilio vyatanda Cameroon maporomoko ya ardhi yakitokea

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wengi wanahofiwa kufa na wengine kupotea katika mji mkuu wa Cameroon Yaoundé, baada ya maporomoko ya ardhi kuharibu nyumba kadhaa katika eneo la Mbankolo jijini huo.

BBC imeripoti kuwa hali hiyo inafuata mvua kubwa iliyonyesha jijini humo jana Jumapili jioni.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali, vimeripoti kuwa takriban watu 13 wamefariki kutokana na maafa hayo, huku takwimu zikitarajiwa kuongezeka.

Shughuli za uokoaji zinaendelea katika eneo hilo huku idadi ya watu ambao hawajulikani walipo baada ya maafa hayo bado haijafahamika.

Novemba mwaka jana, maporomoko ya ardhi katika mji mkuu huo yaliua takriban watu 14 waliokuwa wakihudhuria maziko.

Nchi jirani ya Nigeria siku ya Jumapili ilitoa tahadhari ya mafuriko katika majimbo kadhaa ikihusisha hii na kuagiza kutolewa hara kwa maji ya Mto Benue ambao hutiririsha maji yake kutokea Cameroon.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live