Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vikosi vya wanajeshi kutoka Kusini mwa Afrika kuondoka Msumbiji

Vikosi Vya Kusini Mwa Afrika (Sadc) Kuondoka Msumbiji Vikosi vya wanajeshi kutoka Kusini mwa Afrika kuondoka Msumbiji

Tue, 26 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Wanajeshi kutoka muungano wa kanda ya kusini mwa Afrika ambao walitumwa kukabiliana na waasi wa Kiislamu nchini Msumbiji wanatarajiwa kuondoka nchini humo kutokana na matatizo ya kifedha.

Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (Sadc) imekuwa ikizingatia ukomo wa bajeti yake, waziri wa mambo ya nje wa Msumbiji amesema.

VerĂ³nica Macamo aliongeza kuwa umoja huo unaamini kuwa Msumbiji iko shwari ikilinganishwa na mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambayo imekuwa ikikabiliwa na makundi yenye silaha kwa miongo kadhaa.

Vikosi vya kijeshi vya Sadc vimekuwa vikijaribu kuzima ghasia nchini DR Congo tangu mwezi Disemba mwaka jana.

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi alisema Sadc inapanga kuondoa vikosi vyake "ifikapo Julai".

Hata hivyo, Bw Nyusi alisema, hii haimaanishi kwamba vita vya taifa dhidi ya makundi ya kijihadi vitakoma.

"Nchi pia zimejitolea kufanya kazi nasi kwa pande mbili, ikiwa ni sawa," aliandika kwenye chapisho la Facebook.

"Kama Wasumbiji tunahitaji kuwa tayari kwa ukweli huu. Tusikengeushwe, jukumu kubwa liko kwetu."

Kundi la waasi lililojihami limeshambulia eneo la kaskazini mwa Msumbiji kwa miaka sita, huku kundi la Islamic State likisema ndilo lililohusika na baadhi ya ghasia hizo.

Uasi huo, ambao umehusisha mashambulizi kadhaa dhidi ya umma na vikosi vya jeshi, ulisababisha majibu ya kijeshi mnamo Julai 2021.

Usaidizi ulikuja kwanza kutoka kwa Rwanda, ambayo ilituma zaidi ya wanajeshi 2,000 nchini Msumbiji, na kisha kutoka Sadc.

Chanzo: Bbc