Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vikosi vya usalama vyawasili katika mpaka na DRC

AC0B6829 9DE8 42BE 8E3E E149F92B2136 W1080 H608 S Vikosi vya usalama vyawasili katika mpaka na DRC

Thu, 19 Jan 2023 Chanzo: Dar24

Serikali nchini Uganda, imepeleka wanajeshi wake mpaka wa Mpondwe unaotenganisha eneo lake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baada ya shambulizi la kigaidi kwenye Kanisa ambapo watu 17 walifariki Januari 15, 2023.

Kwa mujibu wa tarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Kasese inayopakana na Kongo, Joe Walusimbi iliyochapishwa kwenye gazeti moja la kila siku nchini humo, imesema wanajeshi hao wanachunguza mienendo ya waasi wa ADF wanaotaka kuvuka mpaka.

Awali, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Uganda, Fred Enanga alisema kumekuwepo na utekelezwaji wa operesheni za usiku zenye kuleta mashaka, ambazo zimekuwa zikifanywa kwenye meli za mizigo na abiria katika ziwa Albert.

Mapema mwezi Desemba, 2022, Uganda iliwakamata watu kadhaa wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa ADF, waliovuka mpaka na kuingia katika Wilaya ya magharibi mwa nchi hiyo Ntoroko.

Chanzo: Dar24