Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vikosi vya usalama vya Uganda vyafunga ofisi ya chama cha Bobi Wine

Vikosi Vya Usalama Vya Uganda Vyafunga Ofisi Ya Chama Cha Bobi Wine Vikosi vya usalama vya Uganda vyafunga ofisi ya chama cha Bobi Wine

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Maafisa wa polisi na wanajeshi wa Uganda wamefunga ofisi za National Unity Platform (NUP), chama kinachoongozwa na mwanasiasa wa upinzani Bobi Wine.

"Kuna uwepo mkubwa wa maafisa wa usalama katika ofisi zetu huko Kamwokya, na kwa sasa hatuwezi kuzifikia," chama cha NUP kilisema katika chapisho kwenye katika mtandao wa X siku ya Jumatatu.

Bobi Wine pia amesema maafisa hao walivamia makao makuu ya chama na kuwazuia watu kuingia au kutoka nje ya majengo hayo.

Mwanamuziki huyo aliyegeuka kuwa mwanasiasa alisema kwenye mitandao ya kijamii kwamba kizuizi cha maafisa wa usalama kinalenga kusimamisha hafla ya maombi ambayo NUP ilipanga kufanya katika ofisi yake mjini Kampala siku ya Jumatatu.

Maombi hayo yalikusudiwa kwa ajili ya "marafiki waliokufa, waliozuiliwa na kutoweka" wa chama.

Wiki iliyopita, polisi walimpeleka Bobi Wine hadi nyumbani kwake baada ya kurejea Uganda kutoka Afrika Kusini, wakisema kuwa hatua hiyo ilikuwa ni kumzuia kuandaa maandamano.

Pia waliwazuilia makumi ya wafuasi wa Bobi Wine kwa madai kwamba walichochea vurugu na kupanga maandamano haramu.

Bobi Wine amewakosoa maafisa hao wa usalama kwa hatua hiyo, inayoenda sambamba na siku ya uhuru wa Uganda.

“Wanapofanya hivi, watakusanyika bila aibu leo ​​kusherehekea ‘uhuru’ hata wanapokuwa na mwennendo mbaya kuliko wakoloni,” alisema.

Chanzo: Bbc