Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vikosi vya usalama Tunisia vyawaweka chini ya ulinzi

Tunisia Tunisiaaaaaa Vikosi vya usalama Tunisia vyawaweka chini ya ulinzi viongozi wa chama cha Kiislamu

Thu, 7 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Kiislamu cha Tunisia cha Ennahdha kimesema kwamba kiongozi wake wa Baraza la Shura Abdel Karim Harouni alikamatwa jana Jumatano baada ya kuwekwa chini ya kizuizi cha nyumbani tangu Jumamosi.

Taarifa ya chama hicho imesema: Maafisa wa serikali ya Tunisia wamemkamata Harouni mwenye umri wa miaka 63 ambaye pia aliwahi kuwa waziri wa uchukuzi wa Tunisia, bila kutaja sababu.

Hatua hiyo iimechukuliwa saa chache baada ya kukamatwa Mondher Ounissi, mkuu wa muda wa chama chama hicho cha Kiislamu. Kabla ya hapo Hamadi Jebali, katibu mkuu wa zamani wa chama cha Ennahdha na waziri mkuu wa zamani wa Tunisia naye alikuwa amekamatwa na serikali ya Kais Saied kabla ya kuachiliwa huru jana Jumatano.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari, Hamadi Jebali, alikamatwa siku ya Jumanne katika msako wa nyumbani, aliachiliwa huru jana usiku baada ya kuhojiwa kwa saa saba na kitengo cha mahakama kinachohusika na kesi za ufisadi wa fedha.

Mwezi Februari mwaka huu pia, serikali ya Tunisia ilikamata idadi kubwa ya viongozi wa chama cha Ennahdha, akiwemo mkuu wa chama hicho, Rached Ghannouchi, naibu wake Ali Al-Arayedh, na waziri wa zamani wa sheria, Noureddine Bhiri, kwa mbalimbali tuhuma zikiwemo za kula njama dhidi ya usalama wa taifa.

Ennahdha, kilikuwa chama kikubwa zaidi katika bunge lililopita la Tunisia ambalo lilivunjwa na Rais wa nchi hiyo Kais Saied mwezi Julai 2021, hatua ambayo wapinzani wanasema ni mapinduzi dhidi ya demokrasia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live