Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vikosi vya jeshi la Eritrea vyaanza kuondoka Tigray

F7a1d54a 47d3 4d90 A189 126d60e1cbdb Vikosi vya jeshi la Eritrea vyaanza kuondoka Tigray

Fri, 20 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakaazi kutoka maeneo tofauti ya eneo la kaskazini mwa Ethiopia la Tigray wameambia BBC kuwa wanajeshi kutoka nchi jirani ya Eritrea wanaondoka kwa wingi kutoka katika maeneo ambayo wamekuwa wakidhibiti.

Mtu aliyeshuhudia katika mji wa Adwa aliambia BBC kwamba magari ya jeshi la Eritrea yamekuwa yakipita katika mji huo tangu Ijumaa asubuhi.

"Wao [askari] wamekuwa wakisafiri kwa magari mengi," alisema. Akielezea idadi ya askari hao kuwa ni “kama mchwa” mkazi huyo alisema magari hayo yalikuwa yakipiga tarumbeta na askari walikuwa wakiimba.

“Walikuwa wakiimba wakiwa na bendera kwenye magari yao,” aliongeza.

Wakati huo huo, jeshi la shirikisho la Ethiopia lilikuwa likiendelea kulinda viunga vya mji, mkazi huyo alisema.

Kwa mujibu wa makubaliano ya amani kati ya serikali ya shirikisho na chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF), uondoaji wa vikosi vya kigeni na vikundi visivyo vya shirikisho vyenye silaha kutoka Tigray ungefanyika wakati vikosi vya Tigray vitakabidhi silaha zao nzito kwa serikali ya shirikisho.

Mkazi mwingine wa mji wa Aksum pia aliambia BBC kwamba makumi ya magari yanayosafirisha wanajeshi wa Eritrea na silaha yamekuwa yakipita katika mji huo.

"Nimehesabu magari 70, vifaru 12 na vingine vingi. Wanajeshi walikuwa kwenye magari tofauti. Wanakuja upande wa Adwa na kuelekea mji wa Shire," Berihu Kahsay, ambaye alikuwa miongoni mwa wakazi waliokuwa wamejipanga barabarani kushuhudia kuondoka huko allisema.

Vyanzo kadhaa nchini Eritrea pia vimethibitisha kuondolewa kwa wingi kwa wanajeshi na zana za kijeshi. Wanajeshi wa Eritrea walipelekwa nchini humo Novemba 2020 kuunga mkono mashambulizi ya serikali ya Ethiopia dhidi ya wapiganaji wa TPLF huko Tigray.

Vita hivyo vilivyomalizika kwa makubaliano ya amani mwishoni mwa mwaka jana vimeua mamia ya maelfu ya watu na wengine mamilioni kuyakimbia makazi yao na kuwa wakimbizi.

Mashirika kadhaa ya haki za binadamu yalishutumu pande zote, wakiwemo wanajeshi wa Eritrea, kwa kufanya ukatili wakati wa mzozo huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live