Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vikosi vya Umoja wa Afrika vyakabidhi kambi zao nchini Somalia

Vikosi Vya Umoja Wa Afrika Vyakabidhi Kambi Zao Nchini Somalia Vikosi vya Umoja wa Afrika vyakabidhi kambi zao nchini Somalia

Wed, 28 Jun 2023 Chanzo: Bbc

Kikosi cha Umoja wa Afrika (AU) nchini Somalia kimekabidhi kambi tatu zaidi za kijeshi kwa jeshi la Somalia ikiwa ni sehemu ya kujiondoa taratibu kunakotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka ujao.

Mwishoni mwa mwezi Juni mpango huo ni kuwaondoa takriban wanajeshi 2,000 kutoka Somalia.

Makabidhiano ya Jumanne yalifanyika Adale, Mirtaqwa na Hajji Ali, katika eneo la Shabelle ya Kati, vituo ambavyo vilikuwa chini ya udhibiti wa kikosi cha ujumbe wa Burundi.

Kufikia sasa kikosi cha AU kimekabidhi kambi sita za kijeshi, tano kati ya hizo zikiwa katika eneo la Shabelle ya Kati

Kambi ya kwanza, iliyoko katika wilaya ya Heliwa katika mji mkuu, Mogadishu, ilikabidhiwa tarehe 22 Januari.Pia iliendeshwa na vikosi vya Burundi.

Haijabainika ni wanajeshi wangapi wa AU ambao tayari wameondolewa kutoka Somalia.

Somalia imekuwa ikitoa mafunzo kwa wanajeshi wapya nchini Uganda, Ethiopia na Eritrea kuchukua nafasi ya wanajeshi 19,000 wa AU waliowekwa sasa.

Haya yanajiri huku Somalia ikijiandaa kwa awamu ya pili ya mashambulizi makubwa ya kijeshi dhidi ya al-Shabab.

Kundi la wapiganaji lenye uhusiano na al-Qaeda limetoa video mpya inayoonyesha kuhitimu kwa mamia ya wapiganaji wap

Chanzo: Bbc