Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vikosi vya Tigray vyashutumiwa kwa mauaji ya kiholela Amhara

Trigay Mzozoggg Vikosi vya Tigray vyashutumiwa kwa mauaji ya kiholela Amhara

Wed, 12 Oct 2022 Chanzo: BBC

Wakaazi wa eneo la eneo la Amhara nchini Ethiopia ambalo lilichukuliwa tena na wanajeshi wa serikali hivi karibuni wamewashutumu wapiganaji kutoka eneo la Tigray kwa unyanyasaji ikiwa ni pamoja na mauaji ya kiholela.

Wilaya ya Raya Kobo ilishikiliwa kwa wiki tano na vikosi vya Tigray. Wakazi hao walisema kwamba watu wanaoshukiwa kuwa wanaviunga mkono vikosi vya serikali walilengwa.

Pande zote za mzozo kaskazini mwa Ethiopia hapo awali zimeshutumiwa kwa kukiuka haki za kimataifa za binadamu.

Uchunguzi wa pamoja uliofanywa mwaka jana na Tume ya Haki za Kibinadamu ya Ethiopia (EHRC) na Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa ulisema kunaweza pia kuwa na ushahidi wa uhalifu wa kivita.

Unyongaji usio wa kimahakama, utesaji, ubakaji, na mashambulizi dhidi ya wakimbizi na watu waliokimbia makazi yao ulirekodiwa. Hata hivyo, mara kadhaa wamekanusha.

Chanzo: BBC