Vikosi vya Somalia vimechukua usalama wa ikulu ya rais na jengo la bunge la shirikisho katika mji mkuu Mogadishu kutoka kwa ujumbe wa Umoja wa Afrika nchini humo (Atmis) baada ya miaka 16.
Rais Hassan Sheikh Mohamud alisifu jeshi la taifa kwa kuchukua jukumu la usalama la viongozi wa nchi, akisema kuwa hatua hiyo ilionyesha "kupatikana tena kwa uwezo na mamlaka" ya jeshi la nchi hiyo, shirika la habari la Sonna linalomilikiwa na serikali liliripoti.
Hatua hiyo inakuja wakati vikosi vya Somalia vikianza kuchukua majukumu ya usalama wa nchi huku wanajeshi wa Atmis, ambao wamekuwa wakipigana na al-Shabab na kulinda vituo muhimu vya serikali tangu 2007, wakiondoka hatua kwa hatua.
Takriban walinda amani 17,000 wa AU wanatarajiwa kuondoka katika taifa hilo la Pembe ya Afrika mwishoni mwa mwaka ujao