Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vikosi vya Serikali ya Umoja wa Kitaifa kuhitimu mafunzo

5155704839bb7b8f298314c1307b1e18.jpeg Vikosi vya Serikali ya Umoja wa Kitaifa kuhitimu mafunzo

Wed, 20 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAZIRI wa Ulinzi wa Sudan Kusini, Angelina Teny amesema vikosi vya Serikali ya Umoja wa Kitaifa vilivyoundwa baada ya makubaliano ya amani vinahitimu mafunzo mwezi huu baada ya kucheleweshwa kwa miaka miwili.

Makubaliano ya amani yaliyosainiwa na Rais Salva Kiir na naibu wake wa kwanza Dk Riek Machar Teny kutoka upinzani mwaka 2018 yamemelekea kuundwa kwa vikosi vya umoja kati ya vikundi vya upinzani na vikosi vya serikali na kupatiwa mafunzo ambayo yanatakiwa kumalizika kwa kipindi cha mpito ambacho kilimalizika Februari mwaka jana.

Teny amesema kutokana na ukosefu wa fedha na utashi wa kisiasa, vikosi hivyo bado hazijahitimu huku jamii za kikanda, kimataifa pamoja na wachunguzi wa amani wakihimiza vyama kuharakisha mchakato huo.

Waziri huyo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Usalama na Ulinzi ya SPLM-IO alisema vikosi vya umoja wa kitaifa sasa vitahitimu mafunzo hayo kabla ya mwisho wa mwezi huu.

"Kwetu huu ni mwanzo mzuri sana na tunatumaini kabla ya mwisho wa mwezi huu tutaona vikosi vya umoja wa kitaifa.”

“Tumehitimisha mkutano muhimu sana uliojumuisha mimi kama mjumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Mpito, Bodi ya Ulinzi ya Pamoja na Kamati ya Pamoja ya Usalama wa Mpito kujadili kuhitimu kwa vikosi hivi. Tumejadili ratiba ya mchakato huu kwa sababu moja ya changamoto kuu ambazo tumekuwa tukikabiliana nazo ikiwamo ni pamoja na ufadhili wa kuhitimu,” alisema.

Ofisa Mwandamizi wa upinzani, mshauri wa usalama wa Rais Kiir na Mwenyekiti wa Kamati ya Mpito ya Kitaifa (NTC), Tut Gatluak wameahidi kutoa rasilimali zote zinazohitajika kwa ajili ya vikosi hivyo kuhitimu mafunzo.

Chanzo: habarileo.co.tz