Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vikosi vya RSF kuunda serikali katika maeneo vinavyoyadhibiti

RSF SUDAN Vikosi vya RSF kuunda serikali katika maeneo vinavyoyadhibiti

Sat, 16 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vikosi vya Usaidizi wa Haraka vya Sudan (RSF) vimetishia kuunda mamlaka ya utawala katika maeneo yanayodhibitiwa na vikosi hivyo, iwapo 'maadui wao' wataunda serikali ya aina yoyote kwenye maeneo hayo.

Kamanda wa RSF, Mohammad Hamdan Dagalo (Hemedti) amenukuliwa na Reuters akisema hayo na kufafanua kuwa: Iwapo jeshi litaunda serikali, tutaanzisha mara moja mashauriano ya kuunda mamlaka halali ya kiraia katika maeneo tunayoyadhibiti; Khartoum ukiwa mji mkuu wake.

Amesisitiza kuwa, hatua yoyote ya jeshi kuunda serikali ya mpito katika Bandari ya Sudan iliyoko katika pwani ya Bahari Nyekundu itapelekea kugawanyika mapande nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Mwezi uliopita, afisa wa ngazi ya juu katika Baraza la Uongozi la Sudan alisema kuna haja ya kuundwa serikali ya muda katika ngome hiyo ya RSF.

RSF imetoa onyo hilo katika hali ambayo, Jenerali Abdul Fattah al-Burhan, mkuu wa Baraza la Uongozi la Sudan hivi karibuni alitangaza kuwa amevivunja vikosi hivyo vya radimali ya haraka.

Majenerali wa kijeshi wanaopigania madaraka nchini Sudan Al-Burhan alitoa tangazo hilo muda mfupi baada ya Dagalo kusisitiza kuwa, njia bora ya kuhitimisha mapigano nchini humo ni kuviunganisha vikosi vya RSF na Jeshi la Sudan.

Maelfu ya watu wameuawa na maelfu ya wengine wamejeruhiwa, huku zaidi ya milioni nne wengine wakiyahama makazi yao ikiwa ni pamoja na Wasudan zaidi ya milioni moja ambao wamekimbilia nchi jirani kutokana na kushadidi vita na mapigano nchini humo, yaliyoanza tangu Aprili 15.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live