Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vikosi vya DRC vyakosolewa baada ya waandamanaji 43 kuuawa

Vikosi Vya DRC Vyakosolewa Baada Ya Waandamanaji 43 Kuuawa Vikosi vya DRC vyakosolewa baada ya waandamanaji 43 kuuawa

Fri, 1 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) limevikosoa vikosi vya usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa kuua makumi ya waandamanaji waliokuwa wakiandamana dhidi ya vikosi vya Umoja wa Mataifa.

Serikali imesema kuwa takribanI watu 43 waliuawa wakati wanajeshi walipovunja maandamano dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa katika mji wa mashariki wa Goma siku ya Jumatano.

Makumi walijeruhiwa na zaidi ya 150 kukamatwa, akiwemo kiongozi wa madhehebu ya kidini.

Awali mamlaka ilikuwa imeweka idadi ya waliofariki kuwa saba pekee, ikiwa ni pamoja na afisa wa polisi ambaye alikuwa amepigwa mawe hadi kufa.

Katika taarifa, HRW ilisema maafisa "walioamuru matumizi ya nguvu zisizo halali wanapaswa kusimamishwa kazi, kuchunguzwa, na kuwajibika katika kesi za haki na za umma".

Ilisema kuwa wanajeshi hao walionekana kufyatua risasi kwenye umati wa watu ili kuzuia maandamano dhidi ya Umoja wa Mataifa, na kuyataja kuwa "njia mbaya na isiyo halali ya kutekeleza marufuku".

Ilisema ilikuwa imethibitisha video mbili zinazoonesha wanajeshi wakitupa miili nyuma ya lori. Serikali inasema imeanza uchunguzi kuhusu suala hilo.

Chanzo: Bbc