Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vikosi vya Afrika Mashariki kusalia DRC licha ya maandamano

Vikosi Vya Afrika Mashariki Kusalia DRC Licha Ya Maandamano Vikosi vya Afrika Mashariki kusalia DRC licha ya maandamano

Wed, 6 Sep 2023 Chanzo: Voa

Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki siku ya Jumanne walikubaliana kwa kauli moja kurefusha muda wa kupelekwa kwa kikosi cha kijeshi cha kanda mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Uamuzi huo unatokea wiki moja baada ya maafisa wa jeshi la DR Congo kuua watu 43 na kuwakamata waandamanaji 168 waliokuwa wakitaka wanajeshi wa Afrika Mashariki na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kuondoka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Jukumu la kikosi cha kanda lilikuwa limalizike tarehe 8 Septemba, lakini kurefushwa kunamaanisha kuwa wanajeshi wataendelea kusalia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa miezi mitatu ya ziada, hadi tarehe 8 Disemba.

Jumuiya ya Afrika Mashariki ilitoa tangazo hilo siku ya Jumanne, baada ya mkutano wa wakuu wa nchi wa kanda hiyo katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Waziri Mkuu wa DR Congo Sama Lukonde, Waziri wa Masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Uganda Rebecca Kadaga na marais wa Kenya Tanzania, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini.

Viongozi hao walisema "walizingatia hatua muhimu zilizofikiwa na jeshi la kikanda la EAC kuelekea kurejesha usalama mashariki mwa DRC (DR Congo)".

Kikosi cha kikanda kilitumwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mnamo Novemba 2022 kusaidia jeshi la DRC Congo kukabiliana na waasi wenye silaha katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Chanzo: Voa