Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijana watakiwa kujua historia mauaji ya kimbari

935f5517b48cda7a46c2b325ff0ddff7.png Vijana watakiwa kujua historia mauaji ya kimbari

Tue, 13 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

VIJANA nchini wametakiwa kuwa na ufahamu juu ya mauaji ya kimbari ili waweze kuwaelimisha watu wanayapinga.

Rai hiyo ilitolewa na Balozi wa Rwanda nchini India, Jacqueline Mukangira wakati akizungumza na wananchi wa taifa hilo la Afrika Mashariki wanaoishi nchini India ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya 27 ya mauaji ya kimbari yaliyofanyika mwaka 1994 nchini Rwanda.

Alisema vijana wengi wa sasa wanayumbishwa na wapinzani wa mauaji ya kimbari kwa sababu hawajipi muda wa kusoma historia ya taifa lao lilikotoka, wakati wa mauaji hayo na mahali lilipo sasa baada ya mauaji hayo.

“Ikiwa vijana watapata ufahamu wa historia ya nchi yao, itakuwa ngumu kuyumbishwa na wapinzani wa mauaji ya kimbari yaliyogharimu maisha ya Wanyarwanda na kuirudisha nyuma nchi,” alisema.

Mkutano huo uliwakusanya pamoja wananchi wa Rwanda wanaoishi katika mataifa ya India, Bangladesh, Sri Lanka, Maldives na Nepal.

Balozi huyo aliwahimiza wananchi hao kutambua juhudi za serikali ya Rwanda katika kuwaletea wananchi maendeleo, pamoja na kujenga taifa lenye mshikamano na umoja.

Chanzo: www.habarileo.co.tz