Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijana washambulia msafara wa Ruto na kuvunja magari vioo

69375e23477a37e3 Vijana washambulia msafara wa Ruto na kuvunja magari vioo

Sun, 24 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Kundi la vijana lilishambulia msafara wa DP likisema Mumias ni ngome ya chama cha ODM hawataki wheelbarrowIlilazimu maafisa wa polisi kuingilia kati na kukabili kundi hilo huku DP akibadili mkondo wake na kuingia NambaleRuto na kikosi chake hawakujeruhiwa wakati wa rabsha hizo za Jumamosi Oktoba 23Ziara ya Naibu Rais William Ruto Mumias imeshuhudia rabsha huku vijana wakirushia msafara wake mawe.

Vijana waliokuwa wamejihami kwa mawe walishambulia msafara huo katika eneo la Korinda katika barabara ya Busia-Kakamega.

Magari kadhaa yaliharibiwa huku picha zilizopakiwa mtandaoni zikionyesha yamevunjwa vioo.

Kulingana na gazeti la Standard, vijana hao walipinga ziara ya DP na walishambulia msafara wake huku wakiimba nyimbo za kusifu ODM.

Wasafiri waliokuwa wakitumia barabara hiyo walijipata kwenye rabsha hizo na kushuhudia hasara.

Aidha DP Ruto na msafari wake walilazimika kubadili mkono na kuingia Nambale huku wakiacha maafisa wa polisi kukabili genge hilo la vijana.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke