Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijana walipwa Tsh. 20,784 kuhudhuria mkutano wa kisiasa wa Raila

0fgjhs5f5nlkmkncl Vijana walipwa KSh 1000 kuhudhuria mkutano wa kisiasa wa Raila

Thu, 14 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Vikundi vya vijana wanaonekana wakiwa kwenye foleni wakipewa KSh 1000 kila mmoja kutoka kwa mwanamke mmojaRaila alikuwa ameandaa mkutano wa kisiasa katika uwanja wa Kamukunji.

Akiwa kwenye mkutano na vijana wa eneo la Mlima Kenya siku ya Jumanne, Oktoba 12, Raila aliahidi kwamba atahifadhi nafasi nne za uwaziri ambazo atawapa vijana iwapo atakuwa Rais.

Huku wanasiasa wakiendelea kuzuru maeneo kadhaa ya nchi wakijipigia debe, imedaiwa kwamba kuna baadhi yao wamekuwa wakiwalipa vijana ili waweze kuhudhuria mikutano yao.

Wa hivi punde ni Raila Odinga ambaye wafuasi wake walionekana kwenye video wakipokea pesa kwa ajili ya kuhudhuria hafla yake siasa ya kisiasa siku ya Alhamisi ,Oktoba 14.

Kupitia kwenye video ambayo imeenezwa kwenye mitandao ya kijamii, vikundi vya vijana wanaonekana wakiwa kwenye foleni wakipokezwa KSh 1000 kila mmoja kutoka kwa mwanamke mmoja.

Akizungumza kuhusu video hiyo, Wakili Ahmednasir Abdullahi alisema ni ukweli kila kijana aliyehudhuria mkutano wa Raila katika uwanja wa Kamukunji, alilipwa KSh 1000.

" Chama cha ODM kina pesa kweli, yaani kila mtu aliyehudhuria mkutano wa kisiasa wa Raila katika uwanja wa Kamukunji alilipwa KSh 1000," Alisema Wakili Ahmednasir.

Raila amekuwa akizuru sehemu mbali mbali za nchi akipiga kampeni na kufanya mashauriano na viongozi kadhaa kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.

Akiwa kwenye mkutano na vijana wa eneo la Mlima Kenya siku ya Jumanne, Oktoba 12, Raila aliahidi kwamba atahifadhi nafasi nne za uwaziri ambazo atawapa vijana iwapo atakuwa Rais.

" Ni kitu ambacho nimejaribu awali na itaendelea kuwa sehemu ya sera yangu, naahidi kwamba vijana watapewa nafasi za uwaziri katika serikali yangu," alisema Raila.

Vijana pia kupitia kwa katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna walimsihi Raila kupunguza bei ya pombe pindi atakapochaguliwa kuwa Rais.

" Baba, vijana wamesema maisha ni mafupi, wanataka kuyafurahia lakini kafyu imewafungia sana na wanataka pia iondolewe, pia wameniambia kwamba ukiingia serikalini, upunguze bei ya pombe," Sifuna alisema.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke