Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijana wa Kenya waongoza kampeni ya kususia utawala wa Israel

E800A641 7008 4D85 ACBA 902F969BDF3D.jpeg Vijana wa Kenya waongoza kampeni ya kususia utawala wa Israel

Sat, 16 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vijana nchini Kenya wanaongoza kampeni ya kususia bidhaa za utawala haramu wa Israel nchini humo kama njia ya kulalamikia mauaji ya kimbari ambayo yamekuwa yakitekelezwa dhidi ya Wapalestina na utawala haramu wa Israel tangu Oktoba 7.

Makundi kadhaa ya kutetea haki nchini Kenya, yakiongozwa na Harakati ya Wakenya Kwa Ajili ya Palestina, yamekuwa yakipigia debe kampeni ya kususia biashara zinazofungamana na utawala wa Kizayuni wa Israel. Orodha za bidhaa au huduma za mashirika yanayofungamana na Israel yanayopaswa kususiwa zimekuwa zikienezwa katika mitandao ya kijamii nchini Kenya.

Aidha makundi hayo ya kutetea haki yamekuwa mstari wa mbele kuwaelimisha wananchi kuhusu kadhia ya Palestina huku yakitoa wito kwa serikali ya Kenya kuchukua hatua ya kukata uhusiano na utawala wa Israel kutokana na jinai zake dhidi ya Wapalestina.

Kwa mujibu wa Televisheni ya Al Jazeera kampeni hiyo ya kususia bidhaa za Israel Kenya inakumbana na changamoto kutokana na idadi kubwa ya mashirika yanayofungamana na Tel Aviv katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Wakenya wameshiriki katika maandamano kadhaa ya kulaani vita vya maangamizi ya umati vya Israel dhidi ya Gaza ambapo watu wa matabaka mbali mbali wameshiriki.

Miezi miwili ya vita vya Gaza imepelekea Wakenya wengi kushangazwa na kushindwa serikali yao kukosoa ukatili wa Israel dhidi ya Wapalestina.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live