Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijana Wamshinikiza Bilionea Dangote Kuwania Urais

Dangote Ng Aliko Dangote

Mon, 31 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kundi la vijana nchini Nigeria, chini ya mwamvuli wa Bunge la Vijana wa Kaskazini, limetoa wito kwa mfanyabishara tajiri zaidi Afrika Aliko Dangote, viongozi wengine wa wafanyabiashara na wataalamu kuingilia kati uchaguzi wa rais wa 2023.

Vijana hao wanasema kuwa uzoefu wao itasaidia kuleta maendeleo Nigeria.Katika taarifa kundi hilo ambalo lilifadhiliwa na Katibu Mkuu wake Desmond Minakaro na Baraza la Wawakilishi, Mohammed Salihu Danlami alisema watu kama Dangote, Femi Otedola, Mike Adenuga, Akinwumi Adesina, Herbert Wigwe, Ngozi Okonjo Iweala na kadhalika wana uwezo wa kuchukua nafasi ya rais wa Nigeria.

Wanasema wafanyabiashara wanaojua jinsi ya kupata faida sasa wanapaswa kuitawala Nigeria. Hata hivyo seneta Shehu Sani amesema haoni haja ya Bw. Dangote kuingilia siasa na kwamba anamtakaaendelee kuwa maarufu kutokana na utajiri wake.

Isha Fola, Joshua Obera, Jibra'eel na @Sirdotskill walisema kwenye akaunti yao ya Twitter kwamba Dangote na vigogo hawa wa biashara huenda wasiweze kuingia katika vituo vyao vya kupigia kura. Wana mtazamo tofauti sana wa kisiasa kwa biashara kwa sababu mara nyingi hulinganishwa na kila mmoja.

@jibsunnah aliandika: Biashara na siasa ni vitu viwili tofauti, anaweza akafanikiwa kwenye biashara lakini hatujui anaweza kufanikiwa kwenye siasa, bora ajikite tu kwenye biashara yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live