Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vifo vyaripotiwa katika mafuriko Nairobi

Vifo Vyaripotiwa Katika Mafuriko Nairobi.jpeg Vifo vyaripotiwa katika mafuriko Nairobi

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Watu watatu wanahofiwa kufariki kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha kwa saa kadhaa katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Miongoni mwa waliofariki ni afisa wa polisi ambaye alikuwa akiokoa familia zilizokwama katika eneo la Kamukunji, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

Mamlaka bado hazijathibitisha vifo hivyo.

Video na picha zilizoshirikiwa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha madereva wakiwa wamekwama kwenye magari yao huku barabara tofauti zikisombwa na maji ya mafuriko.

Sehemu za Barabara ya Nairobi Expressway, inayounganisha uwanja mkuu wa ndege wa nchi hiyo na mji mkuu, pia zilifurika.

Video zilizochapishwa mtandaoni na madereva zilionyesha magari yakielekezwa kwingine na maafisa wa usalama barabarani.

Wataalamu wa hali ya hewa wamesema mvua hiyo itaendelea katika siku chache zijazo.

Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limewashauri madereva na watu wanaotembea kuwa makini.

Chanzo: Bbc