Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vifo vya watu jijini Bata vyaongezeka

F40cea9f63f74237aaef5657d684b734.png Vifo vya watu jijini Bata vyaongezeka

Thu, 11 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Idadi ya waliofariki kutokana na mlipuko mkubwa uliotokea nchini Equatorial Guinea siku ya Jumapili imeongezeka kutoka watu 31chadi kufikia 98, maafisa wamesema.

Mlipuko huo uliotokea katika kambi ya jeshi mjini Bata, ulisababishwa na silaha zilizohifadhiwa vibaya kulipuka baada ya moto kuwashwa na wakulima wanaoishi karibu na kambi hiyo.

Idadi hiyo imeongozeka baada ya kufanyika zoezi la uokozi lililochukua karibu siku nzima kutoka kwa wahudumu wa kujitolea kutafuta miili iliyofukiwa na vifusi.

Tayari Rais wanchi hiyo, Obiang Nguema amesema kuwa mlipuko huo umetokana na uzembe wa kutohifadhi vizuri baruti kambini humo jambo lililopeleka nyumba nyingi katika mji huo kuharibikam vibaya.

Chanzo: www.habarileo.co.tz