Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vifo vya njaa Kenya: Dereva taksi aliyeangukia uchungaji ni nani hasa?

Kanisa Tata Vifo Mchungaji.png Vifo vya njaa Kenya: Dereva taksi aliyeangukia uchungaji ni nani hasa?

Tue, 25 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ulianza kama ufichuzi ambao ungeyeyuka baada ya muda mfupi wa mihemko na lalama.

Lakini kilichoanzia kati kati yam situ eneo la Malindi Pwani ya Kenya wiki moja iliyopita sasa kinageuka kuwa donda ambalo kumbukumbu zake hazitafifia hivi karibuni .

Ufukuzi wa makaburi ya kina kifupi ambapo umetoa miili ya makumi ya watu na kufikisha hadi takriban watu 70 ambao walikufa kwa kuamrishwa kufunga ili kukutana na Yesu.

Muenezaji mkuu wa ‘injili’ hii potofu ni Paul Makenzi-Jina ambalo katika eneo hili linazua hofu na hamu ya kutaka kujua mengi kumhusu .

Vyombo vya habari vya ndani vimekuwa vikijaribu kupekua historia yake ili kumfahamu vizuri na safari yake ilivyoanza kupitia kanisa lake la Good News International hadi kufikia sasa ambapo ameshikiliwa na polisi na kuacha mtiririko wa machozi wa familia ambazo jamaa wao waliokuwa wafuasi wake wameishia kufa au kudhoofika kiafya kwa hatua inayotoshia Maisha yao . Ni nani na alianzaje? th

Chanzo cha picha, Reuters

Mengi kumhusu yanaendelea kujitokeza pindi siku zinavyosinga mbele lakini kuna ya msingi hadi sasa tunayofahamu kumhusu mhubiri huyu tata .

Paul Makenzi alianza Maisha katika la Kilifi kama dereva wa teksi.

Wengi waliomfahamu wakati huo hawakuweza kutabiri kitakachotokea miaka mingi baadaye ambapo simulizi zao ni kama za filamu inayotumbukia kuwa ya kutisha.mwaka wa 2003 wakati kanisa lake lilipoanza kuwavutia wengi ,alibadilisha mafunzo na akaanza kuwataka waumini kuchoma vyeti vyao vya utambulisho na elimu .

Pia wengi waliowahi kuhudhuria kanisa lake wanasema alianza kuhubiri chuki dhidi ya dini nyingine nah apo aliwapoteza baadhi ya waumini wake .

Katika kanisa lake ,Watoto hawakuruhusiwa kwenda shule wala kutibiwa hospitalini .

Haijulikani ni lini hasa alianza kuwataka wafunge ili kukutana na Yesu lakini huenda hilo litatambulika wakati uchunguzi wa miili iliyofukuliwa katika msitu wa Shakhola utakapofanywa na kubaini ilizikwa lini .

Kufikia wakati huo, Makenzi alikuwa ameanza kuikera mamlaka juu ya mafundisho yake makali na yenye msimamo mkali, na alilazimika "kufunga" kanisa lake mnamo 2019.

Hata hivyo, alidumisha ufuasi mkubwa na aliendelea na shughuli za kanisa lake kwa njia tofauti .

Alikamatwa mara kadhaa na ana kesi nyingi ambazo hazijakamilika katika Mahakama za Sheria za Malindi.

Baadaye Makenzi alidai kwamba alifunga kanisa lake baada ya kutimiza unabii wake wa nyakati za mwisho kama alivyoagizwa na Mungu.

Kilichoanza kama uvumi kwamba Makenzi alihamia eneo la Shakahola na kununua ardhi, ambayo wafuasi wake walikuwa wakilima, wakisubiri ujio wa Yesu Kristo kimegeuka kuwa ukweli wa kutisha huku picha za miili ya watu wakifukuliwa zikiwatamaushwa wenyeji na taifa zima Uchungu wa kushuhudia uvundo wa maafa th

Chanzo cha picha, EPA

Takriban makaburi 14 ya halaiki yamechimbwa hadi sasa na Hussein Khalid amekuwa akiangalia watu wakifukua makumi ya miili.

"Harufu ni mbaya na haiwezi kuvumilika," anaiambia BBC.

Waliofariki - sasa wanafikia zaidi ya 70 - wanadhaniwa walikuwa washiriki wa Kanisa la Good News International Church. Inaaminika walishawishiwa kufunga ili wafike mbinguni kabla ya kile walichoambiwa kuwa ndio mwisho wa dunia.

Bw Khalid anaendesha shirika la kutetea haki za binadamu la Haki Africa, ambalo lilipeleka mamlaka kwenye maeneo ya makaburi mwishoni mwa juma lililopita baada ya kufahamishwa na baadhi ya wenyeji.

Mahali hapa "pamefichwa kabisa" ndani ya msitu wa Shakahola na anasema kwamba yeye na timu yake walihitaji kukata vichaka ili kuendesha gari huko.

Miili 39 imetolewa hadi sasa lakini polisi wanasema kuwa 58 wamefariki huku baadhi ya waliookolewa wakifariki dunia wakitibiwa.

Idadi ya mwisho inaweza kuwa kubwa zaidi kwani Shirika la Msalaba Mwekundu limesema kuwa watu 112 wameripotiwa kupotea.

Bw Khalid anakadiria kuwa kuna takriban maeneo 60 ya makaburi ya halaiki katika eneo hilo na ni moja tu ya tano kati ya hayo ambayo yamechunguzwa.

Polisi wanasema kuwa manusura 29 wamepatikana kufikia sasa, lakini inaonekana si wote walitaka kuokolewa, hivyo walikuwa na uhakika kwamba walikuwa na kile walichoambiwa kuhusu mwisho wa dunia.

Siku ya Jumapili, Bw Khalid alikutana na mwanamke mwenye umri wa miaka 20 hivi "aliyeonekana dhaifu sana" .

Lakini hakutaka kusaidiwa.

"Tulipojaribu kumpa huduma ya kwanza ili kumnywesha maji yenye glukosi kwa kijiko, alikataa kabisa. Alifunga mdomo wake na alikuwa akiashiria kuwa hataki msaada wowote," Bw Khalid anasema, akiongeza kuwa mwanamke huyo sasa alikuwa akitibiwa hospitalini.

Pia alikutana na mwanamume mwenye umri wa miaka 40 ambaye aliweza kuongea.

"Alisema hakuhitaji akiba yoyote, na kwamba alikuwa timamu na anajua anachofanya na anapaswa kuachwa peke yake. Hata alituita maadui zake kwenda mbinguni."

Mtu huyo pia amepelekwa hospitali.

Victor Kaudo kutoka Kituo cha Haki za Kibinadamu cha Malindi, ambacho kinasaidia kufukua miili hiyo, anasema anadhani kuna takriban miili 150.

Alisema shirika lake lilipigiwa simu na mtoa taarifa aliyetaka kusaidiwa kuwaokoa watoto wake watatu.

"Ilikuwa bahati mbaya sana kwa sababu tulimwokoa tu mmoja ambaye tulimpata ndani ya nyumba, akiwa amefungwa kwa kamba," aliiambia BBC.

"Na mtoto huyu tunaamini kuwa ana umri wa miaka sita. Lakini dada yake na kaka yake walikuwa tayari wamekufa na walikuwa wamezikwa siku iliyopita kabla hatujafika huko." Maswali mengi kuliko majibu

Kando na msitu wenyewe, kuna mshtuko nchini juu ya jinsi watu kadhaa wangejiua kwa njaa hadi kufa.

Kenya ni nchi yenye dini nyingi na 85% ya watu wanajitambulisha kuwa Wakristo.

Rais William Ruto, ambaye ni mcha Mungu mwenyewe, amemtaja mkuu wa Kanisa la Good News International, Kasisi Makenzie Nthenge, kama mtu ambaye "hakuwa wa dini yoyote".

Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki ametaja kilichotokea kuwa "mauaji".

Mwezi uliopita Bw Nthenge alishtakiwa kuhusiana na vifo vya watoto wawili ambao wazazi wao walikuwa wamejiunga na kanisa lake. Aliachiliwa kwa dhamana, lakini sasa amerudishwa rumande .

Spika wa Seneti, Amason Kingi, alihoji jinsi "uovu wa ukubwa huo wa kustaajabisha [unaweza] kutendeka bila kutambuliwa".

Pia kuna swali la kwanini mtu chakula hadi kufa .

Mwanatheolojia na mwanasaikolojia Dkt James Kipsang Barngetuny aliambia BBC kwamba kulikuwa na tatizo nchini Kenya la "uchakavu" wa makanisa mengi madogo, ambayo hayadhibitiwi ipasavyo.

Alisema kuwa viongozi wasio waadilifu wana uwezo wa kuwavuruga watu akili zao na kutumia azma yao ya kutafuta suluhu ya matatizo yao.

Akiwa amerudi msituni, Bw Khalid ameambiwa kwamba kuna sehemu ya ndani zaidi ambapo watu walikusanyika kusali na amezitaka mamlaka kuharakisha shughuli ya utafutaji na uokoaji katika msitu huo, wa takriban ekari 800 (hekta 325). )

Watu wa eneo hilo wanaanza kuja kwenye maeneo ya makaburi kuwaambia viongozi kuhusu jamaa ambao wamepotea.

Mwanaume mmoja alimwambia Bw Khalid kwamba wanawe watatu, wenye umri wa miaka 21, 17 na 14, walikuwa wamechukuliwa na kaka yake kujiunga na kanisa hilo. Anahofia kwamba wote walikuwa wameaga dunia .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live