Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vifo vya Corona vyapungua kwa 55% Uganda

Image (5)ddr.png Yoweri Museveni, Rais wa Uganda akipatiwa Chanjo ya Corona

Mon, 27 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Utafiti uliofanywa na serikali ya nchini Uganda kupitia mfuko wa Utafiti na Ubunifu katika Chuo Kikuu cha Makerere, umeonesha kuwa idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa Corona imepungua kwa asilimia 55 tangu kuanza kutolewa kwa chanjo dhidi ya ugonjwa huo. \ Nchi hiyo imepoteza watu takribani 3145 hasa katika wimbi la tatu tangu kuzuka kwa ugonjwa huu hatari.

Hata hivyo, katika tafiti iliyofanyika kati ya mwezi Mei hadi Julai mwaka 2021, kuhusu zoezi la utoaji wa chanjo pamoja na wagonjwa 1462 waliokuwa hospitalini wakipatiwa matibabu ya ugonjwa huo walichukuliwa vipimo kwa ajili ya kukamilisha utafiti huo.

Majibu katika utafiti huo yalionesha kuwa asilimia 21 ya wagonjwa walikuwa na umri kuanzia mika 40-49, asilimia 15 wakiwa na umri zaidi ya miaka 70, huku dalili za awali kwa wote zikiwa ni kikohozi, kukosa pumzi na asilimia 51.8 wakiwa wanahitaji huduma ya oksijeni.

"Wagonjwa 95 kati 1462 ambao ni sawa na asilimia 6.5 wamepokea chanjo ya kwanza waliobaki tayari wameshapokea chanjo ya pili, jumla ya ya wagonjwa waliopokea chanjo ni aslimia 55 hawa hawapo tena kwenye hatari ya kupoteza maisha kwa ugonjwa huu, hakuna kifo hata kimoja kwa wagonjwa waliochoma chanjo" imesema ripoti hiyo.

Nae Rais Museven, amethibitisha kupokea chanjo milioni 12 aina ya Johnson&Johnson, AstraZeneca, Sinovac, Sinipharm na Pfizer na kuwataka wananchi wote kuchoma chanjo hizo ili kupambana na kasi ya usambaaji wa viriusi hivyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live