Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Video ya Raila akisakata densi kwenye klabu yachangamsha wanamtandao

29630e7e99c968da Raila Odinga

Thu, 10 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Raila Odinga huwa anachangamsha mwili wakati mwingine na densi kama alivyofanya kwenye video moja

- Wafuasi wake walifurahishwa na video hiyo iliyopakiwa mtandaonu waki hii na wanasema ni wakati wake pia kukulia kwenye kivuli

- Upekuzi wa meza ya TUKO.co.ke hata hivyo umeonyesha video hiyo ni ya mwaka 2019

Video ya kinara wa ODM Raila Odinga akisakata densi imeibuka kwenye mtandao na kuwachangamsha wafuasi wake.

Video hiyo iliyochapishwa kwenye mtandao inaonyesha Raila, anayejulikana kama Baba na wafuasi wake, akiwa kwenye klabu kujivinjari.

Ni klabu ambapo kulikuwa na bendi iliyorindima ngoma zilizomvutia Baba na kuamua kuchangamsha mwili.

Anaonekana kwenye sakafu kabla ya kipusa mmoja kujiunga naye ili wasakate ngoma iliyokuwa ikichezwa.

Raila kuanzia 2018 amekuwa akicheza siasa tofauti baada ya kuingia kwenye urafiki wa kisiasa na Rais Uhuru Kenyatta wa handisheki.

Ni mpango ambao umemuweka kwenye kivuli kisiasa na sasa anafurahia minofu ya serikali kulia na kushoto.

Wakati wa shughuli za maandalizi ya sherehe za sikukuu ya Madaraka iliyofanyika Kisumu, Baba alipeperushwa hadi kaunti hiyo kwa ndege ya kijeshi.

Ni hali ambayo imewaacha wandani wa Naibu Rais William Ruto wakilia na kusaga meno wakisema Raila amechukua nafasi ya DP kwenye serikali.

Kutokana na ufuasi wake mkubwa nchini, wanasiasa wengi wamekuwa wakijihusisha na Baba ili wanufaike.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari kemkem za TUKO hapa

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke