Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vichanga 11 vilivyoteketea Hospitali, Rais amfuta kazi Waziri

Vichanga Moto Vichanga 11 vilivyoteketea Hospitali, Rais amfuta kazi Waziri

Fri, 27 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Senegal Macky Sall amemfuta kazi Waziri wake wa afya Abdoulaye Diouf Zarr baada ya Wwtoto wachanga 11 kufa kwa moto katika chumba cha hospitali cha Watoto wachanga.

Maafisa wanasema hitilafu ya umeme ndio ilisababisha moto kuzuka Jumatano ya wiki hii na kuua Watoto hao wachanga katika hospitali ya mji wa magharibi mwa Senegal wa Tivaouane.

Rais Macky Sall ametoa taarifa ya msiba huo kwenye kurasa yake ya Twitter na kutangaza siku tatu za maambolezo ya kitaifa huku Meya wa mji wa Tivaouane Demba Diop amesema moto huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme na ulisambaa kwa haraka sana. #TanzaniaWeb.Com

Chanzo: www.tanzaniaweb.live