Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viatu vinavyofanana miguu ya binadamu vyaibua zogo mtandaoni

714e5f21efe3dcd9 Viatu vinavyofanana miguu ya binadamu vyaibua zogo mtandaoni

Thu, 15 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Kiatu kisichokuwa cha kawaida kimeibua mjadala moto miongoni mwa wanamtandao

- Katika picha zilizosambaa mitandaoni, kiatu hicho kimetengenezwa kama miguu ya binadamu

- Wengi walionekana kuhisi kwamba kiatu hicho si sawa wengine wakisema kuwa wamependezwa nacho

Ubunifu hutokana na kubuni vitu kwa mtazamo tofauti, lakini kiatu kimewaduwaza wanamtandao.

Mtindo wa kiatu hicho, ambao ulichapishwa kwenye kitandazi cha Twitter na @LifeOfNapaul, umetengenezwa kama miguu ya binadamu.

Mtumizi huyo wa Twitter alionekana kushangaa kuwa kuna aina ya kiatu hicho.

Sawia na aina nyingine ya kiatu, pia imetengenezwa kulingana na rangi tofauti na saizi.

Wengi walionekana kuhisi kwamba kiatu hicho si sawa wengine wakisema kuwa wamependezwa nacho.

Wengine pia walihisi kwamba ni ya kushtua.

@Poshangel8 aliandika: "Ukidhani umeona maajabu kisha unafungua Twitter...Boom!"

@Tarelayefa3: "Hii ni hiy Air Celemax pamoja na mwavuli na ngozi ya JW."

@Samuel4_4: " Kisa mhubiri mmoja atasema tusivae"

@ElizabethBusari: "Ngoja.Wanataka vidole vitoshane na hivyo vya kiatu. Kila mtu ana vidole tofauti."





Kwingineko TUKO.co.ke iliripotia hisia za wanamtandao baada ya mrembo huyo kuzawadiwa kiatu kilichoraruka.

Bella Egooyibo Ubeoyibo Obi, alikuwa amechapsha picha za viatu vilivyoraruka ambavyo mrembo mmoja alizawadiwa.

Kwenye picha hizo, mazungumzo ya Bella na mrembo huyo yalionyesha kuwa alipewa jozi la viatu nane vilivyoraruka.

Mrembo huyo alisema hakuwa amevikagua viatu hivyo kabla ya kuvichukuwa hado alipofika nyumbani na kufungua mzigo huo.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke