Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Veto ya Russia yazima vikwazo vya UN dhidi ya Mali

Veto Power Mali Veto ya Russia yazima vikwazo vya UN dhidi ya Mali

Fri, 1 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Russia imetumia kura yake ya turufu kuzuia pendekezo la Ufaransa la kurefusha muda wa vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Mali.

Vassily Nebenzia, Balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema vikwazo vyote vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Mali vilifikia tamati Alkhamisi ya jana Agosti 31.

Amesema rasimu ya azimio la Ufaransa la kutaka muda wa vikwazo hivyo uongezwe umepuuza kikamilifu wasiwasi ulioonyeshwa na serikali za Bamako na Moscow.

Rasimu hiyo iliyoandaliwa na Ufaransa na Umoja wa Falme za Kiarabu ilitaka vikwazo dhidi ya Mali virefushwa kwa mwak mmoja hadi Septemba mwaka ujao 2024. Vassily Nebenzia, Balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa

Hata hivyo rasimu ya azimio hilo imepigwa na chini kutokana na kura ya veto ya Russia, licha ya kupigiwa kura na nchi 13 wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. China imejizuia kuipigia kura rasimu hiyo.

Kadhalika Baraza la Usalama limepinga rasimu mbadala iliyoandaliwa na Moscow, iliyotaka vikwazo hivyo virefushwa kwa mara ya mwisho kwa kipindi cha miezi 12. Japan imelipigia kura ya hapana pendekezo hilo la Russia, huku nchi 13 wanachama zikijizuia kupiga kura.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live