Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uzalishaji maziwa washuka nchini Kenya

352ed7e6e31d8fe81a65594b05e5867d Uzalishaji maziwa washuka nchini Kenya

Tue, 1 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

UZALISHAJI wa maziwa nchini umeshuka kutoka maziwa ghafi lita milioni 63.4 mwezi Machi mpaka lita milioni 40.2, yanayokusanywa na Bodi ya Maziwa Kenya kutoka kwa wafugaji.

Hali hiyo imesababishwa na mlipuko wa ugonjwa wa covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona ambao umeathiri upatikanaji wa masoko.

Katibu wa Wizara ya Kilimo, Peter Munya, amewataka wafugaji kuongeza uzalishaji na kuwahakikishia upatikanaji wa masoko, akitahadharisha kuwa hali ikiendelea hivyo nchi italazimika kuagiza maziwa kutoka nje ya nchi.

“Baadhi ya wasindikaji wa maziwa hawana maziwa kwa sababu ya wafugaji kupunguza uzalishaji, soko halijaathirika sana kwani wananchi wanaendelea kutumia maziwa hivyo kutishia nchi kuanza kuagiza maziwa nje ya nchi,” alisema Munya wakati wa mkutano wa wadau wa maziwa.

Kenya ni miongoni mwa nchi zenye uzalishaji mkubwa wa maziwa Afrika, ikizalisha lita milioni 5.2 kwa mwaka, huku wafugaji wadogo wakizalisha lita milioni1.8 na kuajiri watu milioni 1.2 .

Mapema mwaka huu, serikali iliamuru kiwanda cha kusindika maziwa cha serikali cha KCC kununua maziwa kwa wafugaji kwa Sh 33 kwa lita, ikiwa ni zaidi ya Sh 25 kwa bei ya awali kwa lengo la kuboresha kipato cha wafugaji.

Chanzo: habarileo.co.tz