Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwindaji haramu wa vifaru waongezeka

Uwindaji Haramu Wa Vifaru Waongezeka Uwindaji haramu wa vifaru waongezeka

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Idadi ya vifaru waliouawa mwaka 2023 nchini Afrika Kusini imeongezeka sanjari na uwindaji haramu. Mwaka jana, vifaru 499 waliwindwa, ikiwa ni ongezeko la vifaru 51 kutoka mwaka uliopita, Waziri wa Mazingira, Barbara Creecy ameeleza.

Afrika Kusini ni nyumbani kwa vifaru wengi duniani. Nchi hiyo ina takribani vifaru weusi 2,000, na karibu vifaru weupe 13,000, wanaotajwa kuwa hatarini.

Pembe za vifaru zimekuwa zikihitajika sana katika nchi za Asia kama vile China na Vietnam, ambapo hutumiwa katika dawa za jadi. Wanyama wengi waliouawa mwaka jana walikuwa katika Hifadhi ya Hluhluwe-iMfolozi katika jimbo la KwaZulu-Natal.

"Ongezeko hilo linatia wasiwasi sana," msemaji wa kampuni inayoendesha hifadhai ya Hluhluwe-iMfolozi Park, Musa Mntambo, aliambia BBC.

Mwaka jana, serikali ilitenga dola za kimarekani milioni 2.1 kuboresha uzio katika Hifadhi ya Hluhluwe-iMfolozi.

Mntambo anasema hatua nyingine kadhaa zimechukuliwa kupambana na ujangili, ikiwa ni pamoja na kuajiri askari zaidi ya kumi na wawili na kupata helikopta mpya ya ufuatiliaji.

Creecy anasema idara yake inafanya mpango mpana wa kuondoa pembe za vifaru, na kuwafanya vifaru hao wasivutie kwa wawindaji haramu. Pia inafanya harakati za kupambana na ufisadi ili kuzuia maafisa wa mbuga hiyo kushirikiana na magenge.

Chanzo: Bbc