Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwanja wa ndege Libya wafungwa

Kufungwaaaaasa Uwanja wa ndege Libya wafungwa

Fri, 10 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mitiga katika mji mkuu wa Libya umefungwa kutokana na mizozo ya kivita iliyokumba maeneo ya karibu na uwanja huo.

Vyombo vya habari vya Libya vimetangaza kufungwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mitiga wa Tripoli, mji mkuu wa nchi hiyo, na kuhamishiwa safari za ndege za kimataifa na za ndani kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Misrata kutokana na machafuko na hatari za kiusalama karibu na uwanja huo.

Televisheni cha al Masar nchini Libya imezinukuu mamlaka za Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mitiga zkitangaza kufungwa uwanja huo na kuhamisha Misrata safari za ndege za ndani na za kimataifa. Misrata ni mji muhimu na uko umbali wa kilomita 200 kutoka Tripoli. Ndege za ndani na za kimataifa zimezuiwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Mitiga jijini Tripol Libya kwa sababu za kiusalama

Kwa upande wake, Mamlaka za Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Misrata zimetangaza kuwasili baadhi ya ndege kwenye uwanja huu kutokana na kufungwa kwa Uwanja wa Ndege wa Mitiga wa mji mkuu Tripoli.

Katika upande mwingine, vyanzo vya ndani vya Libya vimeripoti kwamba, kulikuwa na mapigano ya silaha kati ya makundi hasimu karibu na uwanja wa ndege wa Mitiga.

Hivi sasa Libya inatawaliwa na serikali mbili, moja ni ya Fathi Ali Abdul Salam Bashagha anayejulikana kwa umaarufu wake wa "Fathi Bashagha" na ambaye alipata kura ya imani kutoka kwa Bunge la Libya mwezi Machi mwaka jana, na ya pili ni Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo msingi wake ni makubaliano ya kisiasa yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa. Serikali hiyo ya Abdul Hamid al Dbeibah iliundwa zaidi ya mwaka mmoja nyuma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live