Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uturuki yaafiki kulinda mipaka ya baharini Somalia kwa miaka kumi

Rais Wa Somalia Uturuki yaafiki kulinda mipaka ya baharini Somalia kwa miaka kumi

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la Mawaziri la Somalia limeidhinisha mkataba wa miaka 10 wa ulinzi kati ya Somalia na Uturuki ili kulinda mipaka ya baharini ya Somalia. Bunge la Shirikisho la Somalia nalo pia limetangaza kuafikia mapatano hayo.

Vyombo vya habari vya Somalia viliripoti hapo awali kwamba serikali ya Somalia imeshapitisha mkataba wa usalama wa baharini na Uturuki, ambao unaipa Ankara "mamlaka kamili" ya kulinda na kutetea eneo lote la bahari la Somalia.

Chini ya mkataba huo, Uturuki itapokea 30% ya faida kutokana na shughuli katika ukanda wa kipekee wa kiuchumi baharini nchini Somalia, ambao unajulikana kwa utajiri wake wa rasilimali za kibaolojia. Mkataba huo unatilia maanani sana kupambana na ujangili katika maji ya Somalia.

Katika chapisho tofauti kwenye X, Waziri wa Habari, Utamaduni na Utalii wa Somalia Daud Aweis alisema kwamba, "Bunge la Shirikisho la Somalia pia limeridhia makubaliano ya msingi ya ulinzi na uchumi kati ya Somalia na Uturuki." Amesema makubaliano hayo yanaashiria enzi mpya ya matumaini kwa Somalia na inatumika kama nguvu ya kuleta utulivu. kwa Pembe ya Afrika."

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amesema Uturuki italinda eneo la bahari la Somalia kwa miaka kumi chini ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya Mogadishu na Ankara, na nchi hizo zitaunda jeshi la pamoja la wanamaji.

Mohamud alisisitiza kuwa makubaliano hayo hayalengi nchi yoyote, ikiwemo Ethiopia.

Makubaliano hayo yalitiwa saini wakati wa mvutano mkali kati ya Somalia na Ethiopia, ambayo mnamo Januari ilitia saini mkataba wa makubaliano na eneo lililojitenga la Somaliland ambalo liliruhusu taifa hilo la Pembe ya Afrika kupata njia ya bahari na uwezo wa kuanzisha jeshi la majini. .

Mnamo Januari 6, Rais wa Somalia alilitia saini sheria ya kubatilisha mkataba wa maelewano kati ya Somaliland na Ethiopia.

Somalia inasema, Somaliland ni sehemu ya ardhi yake isiyoweza kutenganishwa na ardhi nyingine za Somalia, hivyo makubaliano hayo hayana nguvu za kisheria.

Umoja wa Afrika umezitaka nchi hizo mbili kuheshimu kanuni za msingi za AU na sheria za kimataifa katika uhusiano wao wa pande mbili na kimataifa. Vile vile umezitaka pande za kigeni kuchunga sheria na kutoingilia masuala ya ndani ya nchi hizo mbili wanachama wa AU.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live