Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utulivu warejea Nairobi

Utulivu Nairobiii Kurejea (600 X 343) Utulivu warejea Nairobi

Tue, 21 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

HALI ya utulivu imerejea katika Wilaya ya Kati ya Kibiashara jijini Nairobi baada ya maandamano ya siku ya Jumatatu ambayo yaliathiri biashara na huduma muhimu za kijamii hivyo kupelekea idadi ya wafanyabiashara kadhaa kuhesabu hasara kutokana na uharibifu uliotokana na vurugu za waandamanaji.

Maandamano ya Jumatatu yalishuhudia polisi wa kukabiliana na ghasia wakiwadhibiti mamia ya vijana waliokuwa wakirusha mawe kwa muda wote wa siku.

Mtandao wa Star Kenya umeripoti kuwa maeneo mengi kati kati ya jiji la Nairobi yalikuwa yamerejea katika shughuli zake za kawaida. Hapakuonesha tishio la usalama na maafisa wa doria wa kawaida walionekana mtaani.

Vizuizi vya muda vilivyokuwa vimewekwa kwenye sehemu za kuingilia Ikulu vimeondolewa.

Polisi bado hawajatoa tamko kuhusu idadi kamili ya waliojeruhiwa na kukamatwa kutokana na maandamano katika maeneo mbalimbali nchini.

Naibu Rais Rigathi Gachagua alisema maandamano hayo yamechangia hasara ya zaidi ya Sh za Kenya bilioni 2 kutokana na kufungwa kwa biashara siku ya Jumatatu.

"Wafanyabiashara kadhaa hawakufungua maduka kutokana na hofu ya waporaji wanaotishia biashara. Kufikia sasa, nchi imepoteza mabilioni kwa maandamano haya kote nchini," Gachagua alisema huku akimtaka kiongozi wa Azimio Raila Odinga kusitisha maandamano hayo.

Raila alitangaza maandamano hayo ili kutoa shinikizo kwa serikali kushughulikia maswala yao kuhusu gharama ya juu ya maisha na kufunguliwa kwa seva za IEBC akidai uchaguzi wa 2022 uliibiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live