Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utawala wa kiraia waungwa mkono na kiongozi wa maandamano Mali

970f39204bed4327ba06d4d84de83a3f 18?fit=500%2C281 Utawala wa kiraia waungwa mkono na kiongozi wa maandamano Mali

Thu, 10 Sep 2020 Chanzo: dar24.com

Imam mwenye ushawishi mkubwa nchini Mali Mahmoud Dicko ameutaka uongozi wa jeshi nchini humo kukubaliana na madai ya viongozi wa mataifa ya Afrika magharibi kumteua rais raia pamoja na waziri mkuu ifikapo Septemba 15 ili kupunguza vikwazo vilivyowekwa baada ya mapinduzi mwezi uliopita.

Hatua hiyo imekaribishwa na mataifa 15 wanachama wa jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika magharibi ECOWAS, lakini vikwazo vimeendelea kuwapo.

Itakumbukwa siku ya Jumamosi uongozi huo wa kijeshi ulianza mazungumzo na vyama vya kisiasa nchini Mali pamoja na makundi ya asasi za kiraia kuhusiana na hatua za mpito kuelekea utawala wa kiraia.

Mwarobaini wa kusaidia wakulima na walaji huu hapaDicko, mhubiri wa nadharia za Kisalafi katika dini ya Kiislamu ambaye mapema mwaka huu alichochea maandamano wakati wa maandamano ya kuipinga serikali, aliliambia shirika la utangazaji la taifa hilo jana kuwa Mali inahitaji msaada na kwamba haina itakachopata kwa kwenda kinyume na jumuiya ya kimataifa.

Kiongozi wa upinzani akamatwa – BelarusMaalim Seif atakavyopambana na wanaompinga

Chanzo: dar24.com