Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utawala wa kijeshi Mali wakanusha madai ya mauaji ya raia

Utawala Wa Kijeshi Mali Wakanusha Madai Ya Mauaji Ya Raia Utawala wa kijeshi Mali wakanusha madai ya mauaji ya raia

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: Voa

Utawala wa kijeshi nchini Mali siku ya Jumatatu umekanusha shutuma ambazo wamesema "zisizo na msingi" zilizotolewa kundi la kutetea haki za binadamu kuwa wanajeshi wake na mamluki wa Russia waliwauwa raia 40 katika operesheni tatu.

Mjini Bamako, wizara ya mambo ya nje ilisema ripoti ya Human Rights Watch (HRW) iliyotolewa wiki iliyopita ilikuwa na "hisia zenye mtazamo wa upendeleo" na kuliweka jeshi la taifa "katika ngazi sawa na makundi ya Kiislamu yenye silaha."

Pia kwa mara nyingine tena, ilikanusha kufanya kazi na kampuni ya kijeshi ya Wagner ya Russia, bila kuitaja. HRW imesema kati ya mezi Aprili na Septemba, makundi ya Kiislamu yenye silaha na wanajeshi wa Mali wamewaua takriban raia 175, wengi wao wakiwa watoto, ikilaani mauaji hayo yaliyowalenga raia kuwa ni uhalifu wa kivita.

Kundi la Support Group for Islam and Muslims lenye uhusiano na Al-Qaeda linahusika na vifo vya takriban raia 135 katika mashambulizi mawili, Shirika hilo lenye makao yake New York lilisema.

Wanajeshi wa Mali na wapiganaji wanaoonekana kutoka Wagner waliwaua raia 40 katika operesheni tatu zilizofanyika kati ya mwezi Aprili na Septemba, lilisema shirika hilo. Viongozi wa kijeshi wa Bamako walianzisha ushirikiano na Wagner baada ya wanajeshi wa Ufaransa kuondoka nchini Mali mwaka 2022.

Ripoti ya HRW ilitokana na mahojiano ya simu kwa watu 40 yaliyofanyika kati ya mwezi Agosti na Septemba. Mamlaka zinasema zinafuatilia kuheshimiwa kwa haki za binadamu na kufanya kuchunguza pale inapobidi, lakini matokeo huwa hayatangazwi hadharani.

Chanzo: Voa