Wed, 28 Feb 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Utawala wa kijeshi nchini Guinea umemteua waziri mkuu mpya, siku nane baada ya kuivunja serikali wakati shughuli katika mji mkuu Conakry zikiwa zimesimama kufuatia siku ya pili ya mgomo wa kitaifa wa wafanyakazi.
Katika hotuba ya televisheni, msemaji wa utawala huo wa kijeshi unaoongozwa na Kanali Mamady Doumbouya amesema Amadou Oury Bah, mchumi na aliyekuwa wakati mmoja kiongozi wa upinzani, ameteuliwa kuhudumu kama waziri mkuu na mkuu wa serikali.
Waziri mkuu huyo mpya amepewa jukumu la kushughulikia mvutano na vyama 13 vya wafanyakazi vilivyoitisha mgomo wa kitaifa ulioanza siku ya Jumatatu.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live