Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utawala wa Kijeshi Mali waahirisha uchaguzi wa rais

Utawala Wa Kijeshi Mali Waahirisha Uchaguzi Wa Rais Utawala wa Kijeshi Mali waahirisha uchaguzi wa rais

Tue, 26 Sep 2023 Chanzo: Voa

Utawala wa kijeshi nchi Mali umetangaza Jumatatu kuahirisha uchaguzi wa rais wenye lengo la kurejesha madaraka kwa raia wa taifa hilo la Afrika Magharibi lililokumbwa na wanajihadi.

Uchaguzi huo ambao ulitarajiwa kufanyika mwezi Februari umetangazwa kuahirishwa kutokana na sababu za kiufundi, jeshi limeahidi kutoa ratiba mpya baadaye.

Duru mbili za upigaji kura – awali zilipangwa kufanyika Febaruari 4 na 18, 2024 -- "zitaahirishwa kidogo kwa sababu za kiufundi" msemaji wa serikali, Abdoulaye Maiga alisema katika taarifa yake iliyosomwa kwa waandishi wa habari.

Sababu hizo ni pamoja na masuala yanayohusiana na kupitishwa kwa katiba mpya mwaka huu na tathmini ya orodha ya wapiga kura, alisema.

Pia msemaji huyo alielezea mzozo na kampuni ya Ufaransa ya Idemia, ambayo utawala wa kijeshi inasema inahusika katika mchakato wa sensa.

"Tarehe mpya za uchaguzi wa urais zitawasilishwa baadaye," alisema Maiga.

Mamlaka pia zinakataa kuandaa uchaguzi wa wabunge, uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka 2023, kabla ya uchaguzi wa rais.

Utawala wa kijeshi "umeamua kuandaa, uchaguzi wa rais peke yake ", ilisema taarifa hiyo.

Chanzo: Voa