Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utata wizi wa magari Kenya na Uganda

Carsdddd Utata wizi wa magari Kenya na Uganda

Wed, 6 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miaka saba iliyopita, kulitokea tukio lililoshtua nchi ya Kenya na Uganda, mara baada ya gari ya aina ya BMW iliyokuwa katika msafara wa Rais Kenyatta kuibiwa jijini Nairobi na baadaye kupatikana nchini Uganda.

Vikosi vya usalama na ulinzi viliharakisha zoezi la kuwakamata wezi hao walifanya tukio hilo la ajabu lililoacha mashangao mkubwa kwa wananchi kwani wezi hao walilazimika kuendesha gari hilo wakiwa na pingu mikononi hadi jijini Nairobi.

Inaelezwa kuwa tarehe 1 Oktoba 2021 kulitokea tukio la mauaji kwa dereva aliyetambulika kwa majina ya Ibrahim Omodo wa miaka 23 aliyekuwa akiendesha gari aina ya Toyota Prado.

Dereva huyo alipokea wateja waliompa 'dili' la Shilingi 200,000 kama malipo na kutoa shilingi 60,000 kwa ajili ya mafuta tayari kwa safari ya umbali wa km 100 yaani kutoka katika mji wa Kakamega hadi Chemelil yote iliyopo Jimbo Kisumu.

Baada ya dereva huyo kuondoka na watu hao ambao wanatajwa kuwa ni mwanamke na mwanaume wa makamo, mawasiliano yake ya simu yalikata, na hakuonekana katika 'kijiwe' wanachotumia kusubiria wateja kwa siku kadhaa.

Alipatikana akiwa kauawa katika shamba la Tindiret lililopo jimbo la Nandi akiwa kafungwa mikono na miguu huku akiwa na majeraha yaliyovilia damu maeneo ya usoni yaliyoashiria kuwa alipata mateso kabla ya mauti kumkuta.

Vikosi vya ulinzi na usalama nchini humo vimefanya uchunguzi na kubaini kuwa gari ambayo alikuwa akiendesha dereva huyo kuwa ipo nchini uganda katika eneo la Tororo.

Mfululizo wa matukio ambayo mengi yanadaiwa kufanywa na genge la wahalifu lililopo Magharibi mwa Kenya limegeuka kuwa tishio kubwa kwa madereva wa gari za kukodisha hususiani madereva 'taxi'.

Matukio haya yanafananishwa na tukio la wizi wa gari la msafara wa Rais Kenyatta, ambalo liliibiwa nchini Kenya kisha kupatikana Uganda, maswali mengi yanaibuka kuhusu uhusiano uliopo kwenye wizi wa magari ya kenya na uganda, mtandao wa wezi hao unahisiwa kuwa mkubwa.

Kwa kipindi cha miezi miwili hadi sasa, jumla ya magari 6 yameripotiwa kuibiwa katika yadi za magari pamoja na maegesho ya magari maeneo ya hoteli tofauti tofauti nchini humo.

Sababu inayotajwa hadi sasa kama moja ya kichocheo cha vitendo hivi ni uwepo wa mfumo mbovu wa ukaguzi wa nyaraka katika mipaka ya nchi hizo mbili, huku wezi wengi wakisemekana kutumia njia maarufu kama za 'panya' wakati wa kuvuka mpaka huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live