Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utata urithi wa kiti cha Mfalme wa Zulu

86934c661f234dbba89a24becacc08a8 660x400.jpeg Utata urithi wa kiti cha Mfalme wa Zulu

Mon, 3 May 2021 Chanzo: millardayo.com

Mzozo kuhusu ni nani atakayemrithi marehemu Mfalme wa Wazulu, Goodwill Zwelithini, sasa unaelekea mahakamani, vyombo vya habari vinaripoti.

Mke wa kwanza, Malkia Sibongile Dlamini, anapinga kutekelezwa kwa wosia wa mfalme uliomtaja mfalme ajaye – huku kukiwa na madai kwamba wosia wake wa mwisho huenda ulighushiwa.

Hatua hiyo ya kisheria inakuja siku kadhaa baada ya kifo cha Malkia Shiyiwe Mantfombi Dlamini Zulu.

Alikuwa ameteuliwa kushikilia wadhifa huo tarehe 24 mwezi Machi baada ya Mfalme Zwethilini kufariki kutokana na matatizo yanayohusiana na ugonjwa wa kisukari akiwa na umri wa miaka 72.

Lakini katika kesi ya kupinga uteuzi wa Malkia Mantfombi kama mrithi wa Mfalme, Malkia Sibongile alitaka mahakama kutambua ndoa yake na marehemu Mfalme huyo kuwa halali. Pia anataka kupewa asilimia 50 ya usimamizi wa nyumba zake.

MEI MOSI: “TULIKUJA NA MATARAJIO YAKUONGEZWA, HATA KWA PUNGUZO TUNASHUKURU”

Chanzo: millardayo.com