Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utapiamlo waua maelfu ya watoto Tigray

F505fdb9 6dbb 4882 9e6b Ba28aae05722 Utapiamlo waua maelfu ya watoto Tigray

Thu, 20 Oct 2022 Chanzo: BBC

BBC imebaini kuwa karibu watoto 2,450 waliokuwa na utapiamlo mbaya wamekufa katika eneo la Tigray nchini Ethiopia tangu mwaka jana, huku vita vya wenyewe kwa wenyewe vikiendelea.

Ugunduzi huo unakuja licha ya serikali kuu kuzuia mawasiliano huko Tigray. Katika kipindi cha miaka mitatu kabla ya mzozo huo, jumla ya watoto 508 waliokuwa na utapiamlo mkali walikufa, lakini kufikia mwaka jana idadi hiyo ilifikia zaidi ya 1,900 na karibu 2,500 mwaka huu.

Madaktari wanaamini kuwa takwimu halisi ni kubwa zaidi kwa sababu watoto wengi wagonjwa hawafiki hospitalini kutokana na migogoro na uhaba wa mafuta kwa ajili ya usafiri.

Eneo hilo limekuwa halina mawasiliano kwa miezi mingi, na kusababisha hali mbaya ya kibinadamu, na maelfu ya watu kuuawa, na zaidi ya watu milioni 2 kukimbia makazi.

Siku ya Jumatano, mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, ambaye anatokea Tigray, alionya kwamba kuna "nafasi ndogo sana ya kuzuia mauaji ya kimbari huko Tigray".

Awali, Serikali ya Ethiopia ilimshutumu mkuu wa WHO kwa kutumia vibaya wadhifa wake.

Vikosi vya Ethiopia vinavyoungwa mkono na Eritrea vimekuwa vikipambana na vikosi vya eneo la Tigray kwa karibu miaka miwili.

Picha mpya za satelaiti za majira ya usiku kutoka Nasa, zilizowekwa na BBC zinaonesha jinsi viwango vya mwanga vimepungua katika miji muhimu ya Tigray.

Hii ni dalili kwamba wamekatwa kutoka kwa gridi ya taifa ya umeme - na kusababisha mzozo wa kibinadamu unaozidi kuwa mbaya. Serikali kuu ya Ethiopia inakanusha kuizuia Tigray kupata rasilimali muhimu na misaada.

Chanzo: BBC