Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utapiamlo wakithiri miongoni mwa wanawake katika nchi masikini

Utapiamlo Wakithiri Miongoni Mwa Wanawake Katika Nchi Masikini Utapiamlo wakithiri miongoni mwa wanawake katika nchi masikini

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Idadi ya wanawake wajawazitona wasichana wenye utapiamloimeongezeka kwa 25% kwa miaka 20 iliyopita, linasema Shirika la watoto la Umoja wa Mataifa Unicef.

Nchi masikini zaidi , kama vile Somalia, Ethiopia na Afghanistan, zimeathiriwa zaidi, imebaini ripoti.

Unicef inakadiria kuwa zaidi ya wanawake bilioni moja na vijana wenye umri wa kubalehe kote duniani wana utapiamlo.

Inasema mizozo ya hivi karibuni vikiwemo vita na janga la Covid vimeifanya hali ukosefu wa chakula wanachohitaji kuwa mbaya zaidi.

Unicef imeitolea wito jamii ya kimataifakufanya usalama wa chakula kuwa kipaumbele cha kwanza , ikiw ani pamoja na kusaidia mipaango ya usaidizi wa chakula chenye virutumisho iliyoshindwa.

Imesisitizia kuhusu athari za utapiamlo kwa watoto.

Ripoti ya Unicef ilibaini kwamba wanawake bilioni moja wenye utapiamlo na wasichana "walikuwa na uzani wa chini wa mwili na walikuwa na kimo kifupi" kutokana na tatizo hilo, kulingana na uchanganuzi wa daza za wanawake katika nchi nyingi duniani.

Chanzo: Bbc