Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utapiamlo ulivyo ua watoto 200 Somalia

Watoto Njaa Somalia Utapiamlo ulivyo ua watoto 200 Somalia

Wed, 6 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema kwa akali watoto 200 wamepoteza maisha nchini Somalia kutokana na utapiamlo.

Ripoti ya OCHA imeeleza kuwa, huku nchi hiyo ya Pembe ya Afrika ikishuhudia mgogoro mkubwa zaidi wa uhaba wa chakula kwa mara ya kwanza tokea mwaka 2017, utapiamlo umeua watoto 200 wa Kisomali tokea Januari mwaka huu.

Taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa, ukame umeongezeka kwa kiasi cha kutisha nchini humo kutokana na mvua kukosa kunyesha kwa msimu wa nne mfululizo sasa katika maeneo manane ya nchi hiyo, na hivyo kuziweka mamilioni ya familia za Wasomali katika hatari ya kufa njaa.

Taarifa ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu imeeleza kuwa, ukame umeathiri watu zaidi ya milioni 7, kutoka milioni 6.1 iliyoripotiwa mwezi Mei, huku watu zaidi ya 805,000 wakilazimika kuyahama makazi yao kutokana na makali ya ukame.

Hii ina maana kuwa, karibu nusu ya watu wa Somalia, sawa na zaidi ya asilimia 45 ya wakazi milioni 15 wa nchi hiyo, wanahitaji msaada wa haraka wa chakula.

Wakati ambapo Somalia ilishuhudia kipindi kigumu zaidi cha ukame katika historia yake baina ya mwezi Mei na Oktoba mwaka 2011, karibu Wasomali 20,000 walikuwa wanaaga dunia kila mwezi kutokana na njaa na utapiamlo, hususan katika maeneo ya kusini na katikati ya nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live