Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utapiamlo, uhaba wa chakula vyaitesa Chad

Kambi Wafa Njaa.jpeg Utapiamlo, uhaba wa chakula vyaitesa Chad

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Idadi kubwa ya wakimbizi waliopo nchini Chad wanatajwa kusababisha uhaba wa chakula na uwapo wa utapiamlo kwa watoto nchini humo kutokana na kukosa lishe bora.

Tovuti ya African news imeripoti kuwa idadi kubwa ya wakimbizi nchini humo inasababishwa na mgogoro unaoendelea katika nchi jirani ya Sudan ambao unasababisha maelfu ya Wasudan kuvuka mpaka wao.

“Chad inahifadhi zaidi ya wakimbizi milioni moja, ikiwa ni mojawapo ya idadi kubwa ya wakimbizi barani Afrika na inayokua kwa kasi,”imesema taarifa ya ripoti hiyo.

Idadi ya wakimbizi wa Sudan nchini Chad imeongezeka maradufu katika kipindi cha miezi sita iliyopita, sambamba na jumla ya waliowasili katika kipindi cha miongo miwili iliyopita tangu mgogoro wa Darfur uanze mwaka 2003.

Chad inakabiliana na uhaba mkubwa wa chakula na utapiamlo, hasa miongoni mwa watoto, unaozidishwa na changamoto za hali ya hewa, shinikizo la kiuchumi, kupungua shughuli za kilimo, na mivutano kati ya jumuiya.

Mgogoro wa wakimbizi unazidi kuzorotesha jamii zisizo na uhakika wa chakula, huku watu milioni 2.1 wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula mwaka 2023.

Tathmini ya Dharura ya Usalama wa Chakula Mashariki mwa Chad inaonyesha matumizi duni ya chakula katika asilimia 90 ya wakimbizi wapya.

Mpango wa Chakula Duniani (WFP) unalenga kusaidia watu milioni 2.85, wakiwemo wakimbizi, IDPs, na wenyeji wanaoishi katika mazingira magumu, kupitia afua za dharura, ulishaji shuleni, na kuzuia utapiamlo na matibabu, ikijumuisha chakula na usaidizi wa pesa taslimu kwa dharura zinazotokea ghafla kama mafuriko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live