Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utapiamlo kwa watoto waongezeka kwa 160% Nigeria - Shirika lisilo la kiserikali

Utapiamlo Kwa Watoto Waongezeka Kwa 160% Nigeria   Shirika Lisilo La Kiserikali Utapiamlo kwa watoto waongezeka kwa 160% Nigeria - Shirika lisilo la kiserikali

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Utapiamlo mkali miongoni mwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kaskazini-mashariki mwa Nigeria Unaongezeka kwa kasi, shirika lisilo la kiserikali limeonya.

FHI 360 ilisema kwamba idadi kubwa ya watoto wenye utapiamlo - 15,781, walilazwa katika vituo vyake kati ya Februari na Septemba kwa ajili ya matibabu, ongezeko la karibu 160% kutoka mwaka jana.

"Hali ya kaskazini-mashariki mwa Nigeria ni mbaya na msaada unahitajika kushughulikia mahitaji muhimu ya kiafya na lishe ya jamii, haswa wanawake na watoto," shirika hilo liliongeza.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, Unicef, limesema hapo awali kuwa Nigeria inashika nafasi ya pili kwa kiwango cha juu cha udumavu wa watoto duniani, ambao unasababishwa na utapiamlo ulioenea hasa katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.

Unicef ​​​​inakadiria kuwa watoto milioni mbili nchini Nigeria wanakabiliwa na utapiamlo, lakini ni 20% tu ya hao hupata matibabu.

Takwimu za Unicef ​​pia zinaonesha kuwa utapiamlo unachangia asilimia 45 ya vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano nchini Nigeria.

Chanzo: Bbc