Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utani wa DP Ruto kwa Rais Uhuru kuhusu kikao cha viongozi wa NASA Mombasa

165db90ae14c17a4 Utani wa DP Ruto kwa Rais Uhuru kuhusu kikao cha viongozi wa NASA Mombasa

Thu, 12 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Ruto alisema haiwezekani waliokuwa wapinzani wa Rais Uhuru ndio kwa sasa amewachagua kuwa marafikiAlisema njama iliyopo ni kutumia afisi ya Rais kwenye safari ya viongozi hao wa NASA kuingia Ikulu 2022Matamshi ya DP yanajiri baada ya Rais kufanya kikao na Raila, Kalonzo, Mudavadi, Wetangula na Moi katika Ikulu MombasaNaibu Rais William Ruto ametania kikao cha Rais Uhuru Kenyatta na waliokuwa viongozi wa NASA kilichofanyika katika Ikulu Mombasa.

Rais alikutana na kinara wa ODM Raila Odinga, naibu wake Wycliffe Oparanya, Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi wa ANC, Moses Wetang'ula wa Ford Kenya na Gideon Moi wa KANU.

Ruto alikashifu kikao hicho wakati wa mkutano wake na wakazi kutoka Ruiru Alhamisi Agosti 12, akisema haiwezekani kwa sasa waliokuwa wapinzani wa Uhuru ndio marafiki.

"Hao watu sita ambao wameenda pale eti kupanga, huyo Rais ambaye wamemtembelea hawajawahi kumpigia kura hata siku moja, hawajawahi kumtafutia kura hata siku moja. Hawajawahi kumsaidia atimize ajenda za Wakenya milioni 45," alisema RUTO.



Read also

"Mengi Yanakuja": Moses Kuria Asema Baada ya Kukutana na Kiunjuri, Martha Karua



Alisema viongozi hao wa upinzani wanaongozwa na maslahi yao ya kugawana mamlaka na ndipo wanamtafuta Rais.

"Wameenda pale ajenda ya kibinafasi, kugawana vyeo na mamlaka," alisema Ruto.

Alisema mpango wa Raila, Kalonzo, Mudavadi na wenzao wanapanga kutumia afisi ya rais kwenye siasa za 2022.

"Eti watumie afisi ya Rais tuliyomsaidia sisi apate eti watuchape sisi. Hiyo inawezekana kweli? Hawa tutawaachia Mungua awakabili," aliongeza DP.

Aliendelea kuwakashifu akisema sasa kazi ya Raila na wenzake ni kupiga kambi Ikulu wakitafuta njia za kubadili katiba ili wapate mamlaka.

"Wanatarajia Uhuru atawasaidia. Baada ya kushindwa kupata vyeo kupitia mabadiliko ya kisiasa, unaona sasa wamevunja NASA. Mpango wao hautafaulu kwa sababu maslahi yao ni ya kujinufaisha," aliongeza.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke