Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utalii washamiri zaidi Kenya

Utalii Washamiri Zaidi Kenya Utalii washamiri zaidi Kenya

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: Voa

Kenya ni moja ya nchi ya Afrika Mashariki ambayo sekta yake ya utalii ndiyo chanzo kikuu cha fedha. Wakati janga la COVID lilipopungua mwaka 2022, ongezeko la fedha liliongezeka kwa asilimia 83 na kufikia dola bilioni 2.13.

Wageni waliongezeka kwa asilimia 72 ya kiwango cha kabla ya janga kutokea mwaka 2019. Waziri wa Utalii Peninah Malonza aliwaambia waandishi wa habari, kiwango hicho kimezipita nchi nyingine barani Afrika ambazo zimebaki katika kiwango cha ukuaji wa asilimia 65 kabla ya janga la COVID.

Kenya inatoa safari za kwenye fukwe zake zilizoko ukanda wa pwani wa bahari ya Hindi na maeneo ya ndani ya kwenye mbuga. Malonza alisema Marekani ilikuwa chanzo kikuu cha wageni katika kipindi cha mwaka 2022. Kenya inafuatiwa na Uganda, Uingereza na Tanzania.

Mapato ya utalii yalitabiriwa kuongezeka mpaka dola 3.37 mwaka huu, alisema David Gitonga, mtendaji mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Utalii inayomilikiwa na serikali, ambapo mapato yanatarajiwa kuongezeka na kufikia dola 4.25 mwaka 2027.

Lakini sekta hiyo pia inakabiliwa na changamoto kubwa , alisema Kareke Mbiuki, mwenyekiti wa kamati ya utalii na wanyamapori katika bunge, akielezea kupunguzwa kwa miundombinu inayohitajika na sekta hiyo ikiwa ni moja ya mpango mkubwa wa serikali wa kubana matumizi. Nchi hiyo pia inakabiliwa na ukame uliokithiri, alisema waziri wa utalii, Malonza.

Chanzo: Voa