Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ushindi wa Bokai wapokewa kwa shangwe Liberia

Ushindi Wa Bokai Wapokewa Kwa Shangwe Ushindi wa Bokai wapokewa kwa shangwe Liberia

Sat, 18 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Wafuasi wa rais mteule wa Liberia Joseph Bokai wamepokea ushindi wa mgombea wao kwa shangwe. Hata kabla matokeo ya mwisho kutangazwa, tayari walishaanza kuingia katika mitaa ya jiji kuu la Monrovia na kushangilia.

Wafuasi wengi zaidi walikusanyika katika makao makuu ya chama chao wakiimba kwa furaha na kumtaka Rais George Weah aliyeshindwa kwenye kinyang’anyiro hicho kukubali kubwaga manyanga.

Wengi wao walikuwa wakiimba kuwa "tumemshinda mcheza densi la Buga” – wakimaanisha Weah ambaye kampeni yake ilipambwa na kibao Buga kilichoimbwa na msanii Kizz Daniel kutoka Nigeria.

Shangwe zaidi zinategemewa kushuhudiwa leo Jumamosi hasa baada ya Rais Weah kukubali matokeo na kumpigia simu Bokai kwa ushindi alioupata.

Chanzo: Bbc