Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ushindani wa Marekani barani utadhuru maslahi ya nchi za Afrika

Ab24ceff5508079b Ushindani wa Marekani barani utadhuru maslahi ya nchi za Afrika

Mon, 3 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Bw. Zhao amesema maslahi ya nchi za Afrika zitadhurika endapo Marekani itafanya ushindani wa nchi kubwa barani Afrika, na kuzifanya nchi za Afrika kuchagua nchi moja kati ya nchi mbili

- Zhao Lijian amesema hayo baada ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken kukutana na marais na mawaziri wa mambo ye nje wa Kenya na Nigeria

- Naye msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika Bw. Robert Godec amesema, Marekani itawaonyesha watu wa Afrika kwamba, ikilinganishwa na mtindo wa maendeleo ya uchumi unaotekelezwa na China barani Afrika, mtindo wa Marekani unazingatia zaidi maslahi ya Afrika

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian leo amesema, maslahi ya nchi za Afrika zitadhurika endapo Marekani itafanya ushindani wa nchi kubwa barani Afrika, na kuzifanya nchi za Afrika kuchagua nchi moja kati ya nchi mbili.

, na kuongeza kuwa anatumai pande mbalimbali za jumuiya ya kimataifa ikiwemo Marekani zitatilia maanani ufuatiliaji wa Afrika, kuchukua hatua halisi kuziunga mkono na uwekezaji, na kuzisaidia nchi za Afrika kukabiliana na changamoto na kutimiza maendeleo.

Zhao Lijian amesema hayo baada ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken kukutana na marais na mawaziri wa mambo ye nje wa Kenya na Nigeria.

Naye msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika Bw. Robert Godec amesema, Marekani itawaonyesha watu wa Afrika kwamba, ikilinganishwa na mtindo wa maendeleo ya uchumi unaotekelezwa na China barani Afrika, mtindo wa Marekani unazingatia zaidi maslahi ya Afrika.

Na Washirika Wetu CRI

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke